Tovuti za Tanzania
AFRICAN STARS BAND (TWANGA PEPETA)
 
 
HAMISI AMIGO(AMIGORAS)- Ni Mtunzi na Muimbaji
Kiongozi wa bendi
 

Nilizaliwa 27 December 1970 mkoani Tabora .
Nilisoma Elimu ya msingi hapohapo na baadae kujiunga na Elimu ya Secondary mpaka Form Six 1989 Nchini Congo(DRC).
  Muziki nilianza zamani kiasi tangu nikiwa shuleni na mwaka 1985 nilijiunga na band ya Normo Net ya nchini Burundi,mwaka 1991 nilirejea nyumbani Tanzania na kujiunga Bicco Stars ya Dar,na kuhamia Chezimba Band ya Dsm 1994 na hapo nilikaa kwa miaka sita hadi 1995 nilipojiunga rasmi na African Stars Band wana wa kutwanga na kupepeta mpaka sasa. 
               
MRS LWIZA MBUTU (NYONI) Muimbaji, Mtunzi na Mcheza show
Kiongozi wa bendi msaidizi
Nimezaliwa tarehe 9February 1973 Jijini Dar es Salaam.
Nilisoma elimu ya msingi na secondar hapahapa Dar na baadae nilijiunga na Course ya Computer na Theory of Music kabla ya
kuingia Chuo cha usimamizi wa fedha IFM kusomea Diploma ya Materials Management, na wakati wote huo nilipenda sana muziki kwani nilianza kwa kuimba katika kwaya mbalimbali za kanisani, lakini katika fani niliingia rasmi 1997 na Band ya kwanza ilikuwa ni Magoma Moto Sound nilidumu kwa mwaka mmoja na 1998 nikajiunga na African Stars mpaka sasa ila pia nimeshawahi kushirikiana na wanamuziki wengine.
SALEHE IDD KUPAZA Muimbaji, Mtunzi na Repa
Nimezaliwa mjini Tanga mwaka 1970. Nilipata elimu yangu ya msingi na Tanga na kumaliza mwaka 1984. Nilijiunga na sekondari na kumaliza mwaka 1988. Mwaka 1990 nilianza rasmi
shuguli za muziki nikiwa na Legho stars, baadae nikaenda Mwenge wana Paselepa. Mwaka 1993 nilienda Tanga nikawa napiga muziki kwenye hotel. Nilienda Nairobi na kujiunga na Less Wanyika mwaka 1994 na hapo mwaka 2000 nilirudi Tanzania nikawa pale Novotel na bendi ya hotelini mpaka mwaka 2001 nilipojiunga rasmi na African stars.

JESSICA CHARLES - Mtunzi na muimbaji

Nilizaliwa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 2 November 1970 Nimesoma mpaka kidato cha nne na kumaliza katika shule ya Secondary ya Kibo mkoani Kilimanjaro 1987,

hata wakati nikiwa shuleni nilipenda sana maswala ya muziki, na katika fani niliingia rasmi 1990 na mwaka huo huo nikajiunga na Matero Band kwa miaka miwili iliyoko Mkoani Dodoma na 1992 nikahamia Band ya Amkeni pia ya hapo Dodoma kwani nilichokuwa nakitaka sikukipata nikahama tena 1993 na kujiunga na Super Melody band ya hapo Dodoma na nilikaa nayo kwa miaka mitatu kabla ya kuelekea visiwani Zanzibar kujiunga na Coconut Band ya Zanzibar mwaka 1996, miaka miwili baadaye nikarejea bara na kutua katika jiji la Dar es Salaam ambapo nilipata nafasi ya kile nilichokuwa nakitafuta, kwani 1998 nikajiunga rasmi na African Stars Band wana twanga pepeta na nipo nao mpaka sasa. 

RAMADHANI MASANGA (BANZA STONE) Muimbaji, Mtunzi na Repa

Nilizaliwa hapo mwaka 1972 na kufanikiwa kumaliza elimu ya msingi katika shule ya Mnazi mmoja Dar es Salaam mwaka 1987. Baada ya hapo nilianza shughuli za muziki na kwenda

kusoma kwenye chuo cha utamaduni cha Korea, Korea Cultural Music Centre kati ya miaka ya 90 na 91. Nilijiunga na Chuo cha Sanaa Bagamoyo mwaka 2000. Kabla ya kuingia chuoni Bagamoyo nilishaanza muziki na kupigia bendi zifuatazo, The heart Strings, Achigo Band kama mpiga drums, Afri-Swez baadaye African Stars. Nilitoka African stars na kwenda Tanzania One theatre TOT na baadae Bambino Sound na hatimaye African Stars Band wana wa kutwanga na kupepeta mpaka hivi sasa.
MSAFIRI DIOUF Muimbaji, Mtunzi na Repa
Coming Soon

CHARLES G. CYPRIAN (Chaz baba) Muimbaji, Mtunzi na Repa

1981 ndiyo mwaka wangu wa kuzaliwa na ilikuwa hapa jijini Dar. Nilipata elimu yangu ya msingi na sekondari lakini niliishia form 2 mwaka 2004. Shughuli za muziki nilizianza tokea nasoma.

 
Nilijiunga na Jandaheka Band ya Bagamoyo baadae Less Bandu. Baada ya bendi hizo mbili nilijiunga na Stone Musika Wajelajela Original. Nikaenda tanga kuanzisha bendi ambayo ilikuwa inajulikana kama Fax Jazz. mambo hayakuwa mazuri nikajiunga na Sot Sound ya Dar baadae nikaenda Mchinga Sound ambako sikukaa sana nikajiunga na African stars wana wa kutwanga na kupepeta mpaka hivi sasa.

KHALID ABDUL CHUMA (Chokoraa) Muimbaji, Mtunzi na Repa

Nilizaliwa pale Bagamoyo mnamo mwaka 1981 nakupata elimu yangu ya msingi hapo Bagamoyo kuanzia mwaka 1991 mpaka 1997. Mambo ya muziki niliyaanza shuleni ambapo nilikuwa katika

vikundi vya kwaya. Mwaka 1998 nilienda Zanzibar kwenye shule ya ufundi na nilipomaliza nilirudi Dar, ambapo nilijiunga na Coconut Band alafu nikaenda Tanga nikajiunga na Mokibo Sound kabla ya kwenda Dar Capital. Nilifanikiwa kwenda Nairobi Kenya kupiga kwenye Mahotel na bendi hiyo na baadae kurudi Tanga. Nilijiunga na Extra Bongo mwaka mwanzoni mwa mwaka jana. Na baada ya hapo nilijiunga na African stars mpaka sasa.
....Next / Endelea....
   
Matangazo
 
     
Home I Management I Biographies I Released Albums I Band Awards
Music Production I News & Events I Zeze Magazine I Contact Us
All rights reserved by ASET
Powered by Benton MEDIA