Tovuti za Tanzania
AFRICAN STARS BAND (TWANGA PEPETA)
 
 
MIRAJI HASSAN SHAKASHIA Sololist

Nimezaliwa mwaka 1974 huko Lushoto Tanga na kupata eleimu yangu ya msingi katika shule ya msingi Mlimani Tanga mpaka mwaka 1991. Baada ya hapo nikaanza kujifunza muziki kwenye

  kikundi cha Makutano Dancing Troupe. Nilijiunga na Zaita Musica hapo mwaka 1992. Mwaka uliofuata yaani 1993 nilijiunga na MK Groupe kwa mwaka mmoja na mwaka 1994 nikaendaVijana Jazz Bendi. Nilirudi tena Tanga na kujiunga na The Golden Sound Band ambayo ilinichukua mpaka Nairobi Kenya. Mwaka 2000 nilijiunga rasmi na The African Stars Band mpaka hivi sasa. 
ALLY AKIDA Guitarlist

Nimezaliwa mwaka 1971 hapa hapa Dar es Salaam na kupata elimu yangu ya msingi katika shule ya msingi Vikawe mkoani pwani mwaka 1979. Sikubahatika kuendelea na elimu ya sekondari

ndipo nilipoanza kujishughulisha na shughuli za hapa na pale mpaka mwaka 1990 ndipo nilipoanza rasmi kujishughulisha na muziki. Mwaka huo huo nikajiunga na Chuma Dancing Troupe, baadaye nilienda Morogoro na kujiunga na Kikundi cha sanaa cha SUA kabla ya kujiunga na Ruaha International hapo mwaka 1993. Mwaka uliofuatia nilijiunga na MCT ( Muungano Cultural Troupe). Baadaye nikaenda Vijana Jazz Band na mwaka 2000 ndipo nilipojiunga na Africanstars wana wa kutwnga na kupepeta hadi leo hii.
ISMAIL KIZUNGA Guitarlist

Mwaka 1975 ndiyo mwaka wa kuzaliwa na nikasoma shule ya msingi Mazinyungu wilayani Kilosa mkoani Morogoro hapo mwaka 1982 na kufanikiwa kumaliza mwaka 1989. Mwaka

1990 niliamia Morooro mjini. Miaka miwili baadaye nilienda Kenya na mwaka 1998 nilikuwa Zibwabwe safari zote hizi ni kwa ajili ya muziki na kujiendeleza zaidi kimuziki. Katika Safari zangu mwaka 2001 nilirudi na kujiunga moja kwa moja na Africanstars mpaka sasa.

JOJO SAIDY JUMANNE Bass Guitarlist

Nilizaliwa tarehe 9 March 1966 Ocean Road Jijini Dar es Salaam Lakini asili yangu ni Mndengereko, nilisoma mpaka darasa la saba katika shule ya msingi Mwananyamala na wakati wote huo nilikuwa

Napenda sana kazi ya Muziki ila kwenye fani hii nimeingia rasmi mwaka 1987 na Band ya kwanza kupigia ni Super Stars ya Mbeya, mwaka 1989 nilienda mjini Dodoma na kujiunga na Band ya Jambo Stars ya mjini hapo ambayo nilikaa nayo kwa muda wa mkwa mmoja tuu kwani 1990nilirudi Dar na kujiunga na Bantu Group, pia sikukaa nayo sana kwani 1992 nilihamia Bicco Stars ya Dar pia na kisha Tanza Musica ya Dar pia mwaka 1995.1996 nilijiunga na Diamond Sound Band kwa kipindi cha miaka minne hadi 2000 nilipoingia katika familia ya African Stars Band wana Twanga Pepeta mpaka sasa   
VICTOR ELIAS MKAMBI Keyboard Player

Nilizaliwa 15 April 1972 Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Tanzania Nimesoma mpaka darasa la saba hukohuko Sumbawanga na baadae nikajiunga na Chuo cha ufundi

Chang'ombe (Chang'ombe Techinical Collage) Dar es Salaam. Nikiwa shule na chuoni nilijihusisha na maswala ya muziki lakini rasmi nimeingia kwenye fani hii mwaka 1990 na Band yangu ya kwanza ni Makondeko Six 1990 nilikaa mpaka 1993 na Band hiyo na kisha nikajiunga na MK Beats Wana Tukunyema 1993 jijini Dar, mwaka 1994 nilihamia Vijana Jazz kwa miaka mitano hadi 1999 nilipojiunga na African Stars wana wa kutwanga na kupepeta mpaka sasa.


THABIT ABDUL (Mtoto wa Ilala)
Keyboard Player

Nimezaliwa tarehe 12/10/1977 Kisarawe Pwani na kupata elimu yangu ya msingi hapa Dar katika shule ya msingi Ananasifu Kinondoni. Nilianza shughuli za muziki na vikundi vya chama kwa

upande wa taarabu. Nilijiunga na TOT mwaka 1999. Nilikaa kwa muda wa mwaka nikajiunga na African stars na baadae kwenda Extra Bongo ambapo napo nilikaa kwa muda wa kama mwaka hivi na hatimaye kurudi tena African stars wana wa kutwanga na kupepeta mpaka hivi sasa.

ABUU SEMUANDO (Baba Diana) Drums

Mimi nilizaliwa 25 October 1952 katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, nilisoma mpaka darasa la nane Middle school hukohuko Muheza na kumaliza mwaka 1965 na niliajiriwa kama karani wa

Daily News mwaka1970 mpaka 1978 na wakati wote huo ndoto yangu ilikuwa kuja kuwa mwanamuziki, na katika fani niliingia rasmi 1979 na band ya kwanza ilikuwa Matimila band ya jijini Dar es Salaam nilikaa nayo miaka miwili na kuhamia Vijana Jazz Band 1982, nilidumu huko kwa miaka 11 na nikajiunga na Tanza Muzika ya Dar pia mwaka 1993 mpaka 1994, baadae nilijiunga na Diamond Sound Band mwaka 1994 mpaka 1997 kabla ya kuingia katika familia ya African Stars Band Wana wa kutwanga na kupepeta mwaka 1998 mpaka sasa.
YAHAYA Drums
Coming Soon
SUDI MCD (CALVIN TIMBO) Paccion Boy

Nilizaliwa tarehe 10 September 1973 Moshi mkoani Kilimanjaro Nilisoma Elimu ya msingi Moshi na kisha kujiunga Elimu ya Secondary Tambaza 1991, mpaka mwaka 1995 nilijiunga na

Bagamoyo College Of Arts nikapata mafunzo ya cheti (Certificate) mpaka 1998 ambapo sasa nikaingia rasmi katika fani ya muziki na band yangu ya kwanza mwaka huo huo ilikuwa Diamond Sound mpaka 2000 nilipohamia African Stars Wana Twanga Pepeta mpaka leo hii.

     
....Next / Endelea....
       
Matangazo
     
 
     
All rights reserved by ASET
Powered by Benton MEDIA