Tovuti za Tanzania
AFRICANSTARS ENTERTAINMENT AWARDS
TUZO ZA AFRICANSTARS ENTERTAINMENT

DAVID MGWASA - TBL
Kutokana na juhudi binafsi za kuipromoti African Stars Band kwa njia mbalimbali.

TBL
Kampuni iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuidhamini African Stars toka ilivyokuwa changa.

OTHMAN MFURU- BAHARI BEACH HOTEL
Kutokana na juhudi zake binafsi,kwa kuilea African stars tokea uchanga wake toka ilipoanzishwa july 1994 mpaka sasa.

RADIO TANZANIA
Redio ya kwanza kuweza kuzipromoti bendi za MK group na MK beats ambazo ndio chimbuko la African stars. Kazi zote zilizofanywa na bendi hizo wakati huo zimerithiwa na African Stars Entertainment ambayo inaendelea kuzisimamia mpaka sasa.

ITV/ RADIO ONE
Moja ya vyombo vya habari vilivyo chini ya IPP limited ambavyo vimechangia kwa kiasi kikubwa kuipromoti African Stars band na African Revolution kwa kuweza kupiga muziki na kuwatengenezea video ambazo huonekana kwenye Televisheni

MWANANCHI/ KITANGOMA
Ni gazeti jipya ambalo nalo liko mstari wa mbele kupromote wasanii mbalimbali.

JOSEPH KUSAGA - MD CLOUDS ENTERTAINMENT
Kwa juhudi zake binafsi tumekuwa naye kwa karibu zaidi toka enzi alipokuwa akiendesha Mawingu(Clouds) Disco pale New Africa Hotel Ghorofa ya Saba wakishirikiana na The Mk Group katika kutoa burdani hotelini hapo, na mpaka sasa akiwa na Clouds Entertainment amesaidia sana kwa njia moja au nyingine kuzipromote bendi zetu za African Stars na African Revolution.

CLOUDS RADIO FM 88.4
Ni redio ambayo inayozipromoti bendi za African Stars, African Revolution na bendi nyingine za Kitanzania kwa kiasi kikubwa sana.

THE GUARDIAN Ltd
Ni kampuni inayo miliki magazeti kama vile Nipashe,Alasiri,The Guardian nk ambayo haiko nyuma pia kupromoti bendi zetu za hapa nchini bila kusahau African Stars na African Revolution

BUSINESS TIMES Ltd
Ni kampuni inayo miliki magazeti kama vile Majira,Dar leo nk ambayo haiko nyuma pia kupromoti bendi zetu.

HABARI CORPORATION
Ni kampuni inayo miliki magazeti kama vile Mtanzania,Bingwa,Rai nk ambayo haiko nyuma pia kupromoti bendi zetu.

UHURU/ MZALENDO
Magazeti ya Uhuru na Mzalendo yameonyesha juhudi zake za kutupromote tokea enzi za MK group na Mk beats.

DAILY NEWS
Magazeti ya serikali ambayo yameonyesha juhudi zake vile vile toka enzi MK group na Mk beats.

DTV/CHANNEL 10
Televisheni zinazopromoti bendi na wasanii wetu katika vipindi kama vile 'Nani ni nani'

TELEVISHENI YA TAIFA - TVT
Televisheni yenye vipindi vinavyopromoti bendi zetu kama vile 'Usiku wa raha'

SHOGHOLO CHALI -BASATA- SECRETARY GENERAL
Katibu wa Baraza la Sanaa la Taifa kwa kutoa ushauri katika kuzijenga bendi zetu na kutupa moyo toka enzi za MK group mpaka sasa tukiwa na African Stars Band na African Revolution Band.

FARAHANI MZEE - CHAMUDATA
Katibu wa CHAMUDATA ambaye ametusaidia kwa kutoa ushauri na miongozo mbalimbali katika kuzijenga bendi zetu toka enzi za MK group mpaka sasa tukiwa na African Stars Band na African Revolution Band.

RADIO UHURU
Kwa kupromoti muziki wetu na bendi zetu za African Stars na African Revolution

RAILWAY CLUB- SINGA SINGA
Ni klabu ya kwanza iliyotukaribisha katika ukumbi wao na kuweza kuzitangaza bendi zetu mjini,baada ya kuhama toka mahotelini ambako tulikuwa tukipiga kama resident bands.

PAPAA MUDDY
Kwa kutoa mchango wake binafsi katika kuzipromote bendi zetu katika kumbi mbali mbali na hasa zilipokuwa zikitumbuiza Railway Club - Singa Singa

MANGO GARDENS
Sehemu ambayo tumekuwa tukiitumia kama ukumbi wetu wa nyumbani na ndipo palipo tupo umaarufu tulionao.

CLUB BILICANAS
Management yao tumekuwa nayo na uhusiano wa karibu katika maswala ya burudani tukishirikiana toka enzi za MK group mpaka hivi sasa tukiwa na African Stars kwenye usiku wa mwafrika.

TCC CLUB
Club ambayo tumekuwa tukishirikiana nayo toka enzi za MK Group, MK Beats na MK Sounds na mpaka hivi sasa tuko nao pamoja tukiwa na African Stars - Twanga pepeta katika kutoa burudani kila siku za jumapili.

MEHBOOB - FKW DISTRIBUTORS
Huyu ni Distributor wetu Amekuwa mstari wa mbele katika usambazaji wa kanda zetu,(video tapes na audio tapes)

CAP KOMBA -TOT
Ni mtu ambaye ametoa changamoto(challenge) katika kufanya muziki wetu uwe wa kiushindani na tunampongeza kwa kuwapeleka wasanii wake shule ili wajaribu kutukaribia kama siyo kutufikia.

MIRAJI SHAKASHIA - AFRICAN STARS BAND
Huyu ni kijana ambaye tumekuwa naye toka angali mdogo katika enzi za MK Group akicharaza Solo Guiter na hivi sasa tunaye akicharaza hilo solo katika Twanga Pepeta.

MSICHOKE KOMBO -AFRICAN REVOLUTION BAND
Huyu naye pia tumekuwa naye akiwa mdogo sana toka enzi za MK Group wakati huo akilicharaza Bass Guiter na hivi sasa anaendelea kulipiga hilo Bass kisawasawa katika bendi yetu ya African Revolution - Tam Tam

VODACOM
Kampuni ambayo imetudhamini katika Uzinduzi wa album yetu ya Chuki Binafsi na tunatumaini kuendelea kuwa nayo pamoja katika maswala ya promotion.

PRIDE COMPUTERS
Kampuni ambayo tumekuwa tukishirikiana nayo kwa karibu zaidi katika kushughilikia utengenezaji wa kazi zetu (Products) hasa upande wa graphic na printing works pia kwa kiasi kikubwa wameshughulikia design ya Website yetu ya mwanzo kabisa

 

   
 
   
Matangazo
   
     
All rights reserved by ASET
Powered by Benton MEDIA