Uzinduzi wa albam ya Safari
2005 Diamond Jubilee
Tarehe 26 mwezi wa nane mwaka 2005 siku ya Ijumaa ilikuwa siku
kubwa sana kwa wanatwanga na kupepeta pale walipozindua albam
yao ya saba katika muziki wa dansi. Siku yenyewe ilikuwa tulivu
sana kutwa nzima na jioni ilipowadia watu walikuwa katika pilika
pilika za kujiupara tayari kwenda kushuhudia kile ambacho kwa
takribani mwezi mzima kilikuwa kinatangazwa kwenye vyombo vya
habari
Nilipata nafasi ya kwenda kushuhudia uzinduzi huo na nilifika
mitaa ya Diamond Jubilee kama kwenye saa mbili na nusu au tatu
kasorobo hivi. Nikajongea kwenye tiketi na kupata tiketi yangu
na mamsapu wangu maana siku hiyo alinipana ile mbaya niende naye
kwani siku zote nilikuwa namkacha safari hii hakukubali. Basi
tukaingia ndani baada ya kuonyesha tiketi zetu mlangoni Muda huo
ukumbi ulishaanza kujaa watu tukaenda mbele kidogo kwa bahati
nzuri tukafanikiwa kupata viti karibu na ukuta ambao unatenganisha
kati ya waliotoa kiingilio cha pili na cha kwanza, cha kwanza
kikiwa ni VIP na cha pili ni kile cha akina sisi.
Kwa kweli kwa wakati huo kulikuwa hakuna bendi yoyote inayoburudisha
ila niliweza kuwaona vijana wa benchmark wakiwa na video kamera
zao huku pembeni mwa kuta za Diamond kukiwa na screen kubwa mbili
ambazo zilikuwa zinaonyesha LIVE nini kinachoendelea pale ukumbini.
Kwa kuwa Onyesho lilikuwa alijaanza basi nikaenda kutafuta cha
kulumangia. Nilirudi kwenye siti yangu tayri kuangalia nini kinachoendelea
na kweli mra akaja MC Maumatha na kuwakaribisha watu wote pale
na kutoa ratiba ya burudani kwa siku hiyo. MC aliwakiribisha wana
African Revolution band wana Diko Diko kuanza kutumbuiza. wana
Diko bila kupoteza muda waliingia na kuanza kuwasha moto. kwa
kweli watu waliwashangilia sana hasa kwa shoo zao ambazo zilikuwa
zimetulia ile mbaya.
Kwa kweli wacheza shoo wa Diko sio mchezo hasa kina Rukia Bruno
na Asha huku Grace na Aliyah nao wakijipinda kama nyoka aina ya
Anaconda. Albam ya hawa African revolution ni hatari yaani kama
haujaipata tafari nenda sasa dukani kabla haijaisha maana unakosa
uhondo. Diko diko waliendelea kwa muda na ilipotimu saa tano kasorobo
hivi mambo yakaanza Mc aliishika kipaza sauti na kumkaribisha
Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka ili naye aseme machache na wakati
huo huo kukaribisha mgeni rasmi ambaye alikuwa mmoja wa wagombea
ubunge katika uchaguzi unaokuja baada ya kukaribishwa naye aliongea
machache na kuizindua albam kwa kuonyesha mfano wa CD ambayo itakuwa
na jina la safari 2005
Wapenzi wa twanga walimshangilia mgeni rasmi na yeye hakutaka
makuu aliomba wana twanga waingie stegini na kuanza kutumbuiza.
Basi kila mtu hakujua nini kinatokea mara tukasikia tututututuutu
tututuuutuuu eh! kila mtu akawa anaangalia huku na huku eh nini
tena hicho mara kwa upande wa kushoto eh skuta pikipiki duh wapigaji
wa twanga wanaingia na Bajaj duh wanaingia wawili wawili, wakiongozwa
na Baba Diana Abuu Semuando huyo kasimama kwenye bajaj kuangalia
vizuri tunamuona MCD naye huyo yupo na mzee wa Bass gitaa Jojoo
jumanne Victor mkambi huyo naye anakuja na bajaj nyingine kwa
kweli pale mbele ya jukwaa ni fujo tupu bajaj zinapiga misele
ndani ya ukumbi mabaunsa wanazunguka huku na huku kuweka ulinzi
mkali duh hawa madereva wa Bajaj ni mafundi sana maana wanapiga
no linda humu humu ndani ya ukumbi kwa kweli ni ajabu sana
Wapigaji wa twanga wanatelemka kwenye hizo Bajaj na kuelekea kwenye
jukwaa tayari kutuletea burudani. watu wanabaki wanashangaa na
kusema ama kweli twanga safari hii wameamua sio mchezo. Linapigwa
sebene pale watu wanatupa macho huku na huku kuangalia nani wanakuja
safari hii, mara kwa upande ule ule wa kushoto wanaingia waimbaji
wa twanga wakiongozwa na akina Chokoraa, Charles Baba, Diouf,
Amigoras, Lwiza Mbutu, Salehe kupaza na Banza Stone ambao wanakuja
kwa staili ambayo hatujawahi kuiona katika maonyesho yao, alafu
kilichopendezesha sasa walikuwa wametilia mavazi meupe yaani suruali
nyeupe na mashati meupe huku wakiwa wameuramba mkanda mweusi ee
bwana ee walitoka bomba ile mbaya na chini wamekula kiatu cheusi
kilichong'arishwa vizuri sana. huku wakiendelea kulisakata sebene
lile watu waliwashangilia sana hasa Banza Stone ambaye alikuwa
anajituma ile mbaya huku Diouf naye akilisakata hilo sebene kwa
makini sana.
Sasa ikaingia zamu ya wacheza show ee bwana ee! kweli hii safari
maana wacheza shoo waliingia na staili ya traffic kwa kweli walipendeza
sana hasa kofia zao na kina dada zile mini sketi zao huku wavulana
wakiwa na nguo nyeupe tupu pamoja na kofia nyeupe, kwa kweli tuliopata
nafasi ya kuona uzinduzi huu tulipata burudani ya kukata na shoka.
Baada ya show hiyo ya traffic twanga walianza na wimbo mpya unaoitwa
Safari ambao umebeba Albam yenyewe ama kweli Twanga ni kisima
cha burudani maana kwa ujumla wanamuzi wote walijituma sana kuonyesha
uwezo wao na kweli tulipata burudani safi sana siku hiyo.
Twanga walipiga nyimbo nyingine tano na watu waliwashangilia sana.
Baada ya nyimbo hizo Twanga walienda kwenye mapumziko kidogo hiyo
ilikuwa kama kwenye saa saba na nusu usiku hivi hapo sasa MC akatangaza
kuwa ni zamu ya baba ya muziki msondo Ngoma kutumbuiza watu walifikiri
utani mara tukawaona hao msondo ngoma wakiingia kwenye stage na
uniform zao bomba nikamuona Mabele akishikilia gitaa la solo na
Ngurumo naye huyo mambo yakaanza wimbo wa talaka yangu utatoa
ndiyo ulikuwa wa kwanza watu walishindwa kujizuia wakavamia kwenye
dancing floor na kuanza kusakata msondo ngoma.
Kweli hawa jamaa wa msondo ni baba wa muziki hapa Tanzania maana
jinsi walivyokuwa wanapiga we acha tu. Msondo walipiga nyimbo
kama tatu hivi na baada ya hapo wana wa kutwanga na kupepeta waliingia
tena jukwaani safari hii walipiga zile nyimbo za albam zilizopita,
walianza na wimbo wa Mtu pesa wapenzi waliivamia dancing floor
na kuanza kutwanga na kupepeta kwa nguvu zote.
Twanga waliendelea kuwapa burudani wapenzi waliofika kwenye uzinduzi
huo mpaka kwenye muda wa sa tisa na nusu hivi ndiyo ikawa mwisho
wa onyesho hilo. Baada ya Twanga kumaliza taratibu nilimvuta mwenzi
wangu tukatoka nje na kwa bahati mabasi yalikuwepo usiku huo tukapanda
basi yaani daladala mpaka mahome UZINDUZI ULIFANA SANA MTU KIBAO.
Picha za uzinduzi huo zinapatikana hapa
|